Wednesday, July 4, 2012

MAJINA 99 YA ALLAH (SW) NA MAANA YAKE

MAJINA 99 YA ALLAH (SW)
Mwenyezi Mungu S.W.T. katuamrisha sisi Waislamu katika Kitabu Chake,
Qurani Tukufu, tumuombe kwa kutumia majina Yake. Kama alivyosema katika
Suratil Israa aya ya 110, “
 دْ عُوا فَلَھُ الأَسْمَاءُ الْحُسْنَ ق ىلُ ادْ عوُا للهَّ أوَْ ادْ عُوا الرَّحْمَانَ أَیًّا مَا تَ …
Maana yake, “Sema: “Mwombeni Allah (Mwenyezi Mungu), au
mwombeni Rahman (Mwingi wa Rehema), kwa jina lolote mnalo mwita.
Kwani Yeye ana majina mazuri mazuri…”
Pia Mwenyezi Mungu S.W.T. kasema katika Suratil A`araaf aya ya 180, “
 الأسَْمَاءُ الحُْسْنىَ فاَدْ عُوهُ بِھَا وَذَرُوا الَّذِینَ یُلْحِدُونَ فِي أَسْمَائِھِ 􀍿 وَ َِّ …
Maana yake, “Na Mwenyezi Mungu ana majina mazuri mazuri;
muombeni kwayo. Na waache wale wanaoharibu utakatifu wa majina
Yake…”
Na Mtume S.A.W. kasema katika Hadithi ilyopokelewa na Abu Huraira
R.A.A. na iliyotolewa na Ahmad, “
تِسِعْةَ وًتَسِعْیِن اسمْاً ، ماِئةَ إًلاِ وَّاَحدِا منَ أَحْصَاھَا دَخَلَ الْجَنَّةَ‘‘ 􀍿 ’إ’نِ ِ
Maana yake, “Hakika Mwenyezi Mungu ana majina tisini na tisa. Majina
mia isipokuwa moja. Atakayeyahifadhi (majina haya na kujua maana
yake) ataingia Peponi.”
Pia Mtume S.A.W. kasema katika Hadithi ilyopokelewa na Abu Huraira
R.A.A. na iliyotolewa na L-Bukhari, “
ِ تِسْعَةٌ وَتِسْعُونَ اسْمًا ، مِائَةٌ إِ‘‘ 􀍿 ’’لاَّ وَاحِدًا ، لا یَحْفَظُھَا أَحَدٌ إِلاَّ دَخَلَ الْجَنَّةَ َِّ
Maana yake, “Mwenyezi Mungu ana majina tisini na tisa. Majina mia
isipokuwa moja. Hakuna atakayeyahifadhi (majina hayo na kujua maana
yake) isipokuwa ataingia Peponi.”
Ingawa Mwenyezi Mungu Mtukufu katuelezea kwamba majina Yake ni tisini
na tisa, lakini hata hivyo majina Yake ni zaidi kuliko hivyo. Hakuna mtu
yeyote yule hapa duniani anayeyajua majina Yake yote isipokuwa Mwenyewe
Muumba wa mbingu na ardhi. Na Majina haya tisini na tisa yanatafsiri sifa
Zake nzuri ambazo sifa hizo hazilingani na sifa za viumbe Wake. Ndio maana
Mwenyezi Mungu S.W.T. katuamrisha wakati tunapotaka kumuomba basi
kwanza kabla ya kuomba dua tumuombe kwa majina hayo, halafu tuombe
tunachotaka kuomba. Na wakati wa kumuomba tuwe katika tohara na moyo na
kiwiliwili vimnyenyekee Mola Mtukufu, wala tusijishughulishe na mambo
mengine.
Ndio maana Mtume S.A.W. kasema,
“Mwenyezi Mungu hapokei dua ya mtu yule moyo wake umeghafilika
wakati anapoomba.”
Na majina hayo tisini na tisa yametajwa na Mtume S.A.W. kama yalivyokuja
katika Hadithi iliyopokelewa na Abu Huraira R.A.A. na kutolewa na Ttirmidhi.
Na anayetaka kuomba dua kwanza asome,
“AUDHU BILLAAHI MINA SHAITAANI RRAJIYM. BISMI LLAAHI
RRAHMAANI RRAHIYM: ALLAAHUMMA INNIY ATAWAJJAHU
ILAIKA BIASMAA-IKAL HUSNAA YAA MAN HUWA, “
للهَّ الذَّيِ لا إلِھَ إلِا ھوَُ ، الرَّحْمنَُ ، الرَّحِیم ، المْلَكُِ ، الْقُدُّوسُ ، السَّلامُ ‘‘
ئُ ، الْمُصَوِّرُ ، الْمُؤْمِنُ ، الْمُھَیْمِنُ ، الْعَزِیزُ ، الْجَبَّارُ ، الْمُتَكَبِّرُ ، الْخَالِقُ ، الْبَارِ
الْغَفَّارُ ، الْقَھَّارُ ، الْوَھَّابُ ، الرَّزَّاقُ ، الْفَتَّاحُ ، الْعَلِیمُ ، الْقَابِضُ ، الْبَاسِطُ ،
الخَْافضُِ ، الرَّافعِ ، المْعُِزُّ ، المْذُلِ ، السمَِّیع ، البْصَِیرُ ، الحَْكمَ ، العْدَْ لُ ،
، ریِبَكْلا ، يِلَعْلا ، روُكَّشلا ، روُفَغْلا ، میِظَعْلا ، میِلَحْلا ، اللَّطِیفُ ، الْخَبِیرُ
الْحَفِیظُ ، الْمُقِیتُ ، الْحَسِیبُ ، الْجَلِیلُ ، الْكَرِیمُ ، الرَّقِیبُ ، الْمُجِیبُ ، الْوَاسِعُ
، يِوَقْلا ، لیِكَوْلا ، الْحَكِیمُ ، الْوَدُودُ ، الْمَجِیدُ ، الْبَاعِثُ ، الشَّھِیدُ ، الْحَقُّ
الْمَتِینُ ، الْوَلِيُّ ، الْحَمِیدُ ، الْمُحْصِي ، الْمُبْدِئُ ، الْمُعِیدُ ، الْمُحْیِي ، الْمُمِیتُ ،
الْحَيُّ ، الْقَیُّومُ ، الْوَاجِدُ ، الْمَاجِدُ ، الْوَاحِدُ ، الصَّمَدُ ، الْقَادِرُ ، الْمُقْتَدِرُ ، الْمُقَدِّمُ
مُؤَخرُِّ ، الأَوَّلُ ، الآخرُِ ، الظَّاھِرُ ، الْبَاطنِ ، الْواَلِي ، الْمُتَعَالِي ، الْبَر ، لا ،
التوََّّابُ ، المُْنتْقَمُِ ، العْفَوُُّ ، الرَّءُوفُ ، مَالكُِ الْمُلْكِ ذُو الْجَلالِ وَالإِكْرَامِ ،
الْمَانِعُ ، الضَّارُّ ، النَّافِعُ ، النُّورُ ، الْھَادِي الْمُقْسِطُ ، الْجَامِعُ ، الْغَنِيُّ ، الْمُغْنِي ،
’’ُرْوُبَّصلا ، دیِشَّرلا ، ثِراَوْلا ، يِقاَبْلا ، عیِدَبْلا ،
ALLAAHU LLADHIY LAA ILAAHA ILLA HUWA (Yeye Ndiye
Mwenyezi Mungu Ambaye hapana mungu isipokuwa Yeye tu),
ARRAHMAANU (Mwingi wa rehema), ARRAHIYMU (Mwenye
kurehemu), AL-MALIKU (Mfalme wa milele), AL-QUDDUWSU
(Mtakatifu, ametakasika na sifa zote chafu), ASSALAAMU (Mwenye
kuleta amani), AL-MU-UMINU (Mtoaji wa amani), AL-MUHAYMINU
(Mwenye kuyaendesha Mwenyewe mambo Yake), AL-`AZIYZU (Mshindi
katika mambo Yake), AL-JABBAARU (Anayefanya analolitaka), ALMUTAKABBIRU
(Mkubwa), AL-KHAALIQU (Muumbaji), AL-BAARIU
(Mtengenezaji), AL-MUSAWWIRU (Mtia sura), AL-GHAFFAARU
(Mwenye kusamehe), AL-QAHHAARU (Mwenye nguvu juu ya kila kitu),
AL-WAHHAABU (Mpaji mkuu), ARRAZZAAQU (Mwenye kuruzuku),
AL-FATTAAHU (Hakimu), AL-`ALIYMU (Mjuzi wa kila kitu), ALQAABIDHU
(Mwenye kunyima au kuzuia), AL-BAASITU (Mwenye
kutoa), AL-KHAAFIDHU (Mfedheheshaji waovu), ARRAAFI`U
(Mpandisha daraja), AL-MU`IZZU (Mtoa heshima kwa amtakaye), ALMUDHILLU
(Mnyima heshima kwa amtakaye), ASSAMIY`U (Mwenye
kusikia), AL-BASIYRU (Mwenye kuona), AL-HAKAMU (Mwenye
kuhukumu), AL-`ADLU (Muadilifu), AL-LLATIYFU (Mwenye kujua
yaliyofichikana), AL-KHABIYRU (Mwenye kujua yaliyo dhahiri), ALHALIYMU
(Mpole), AL-`ADHIYMU (Aliye Mkuu), AL-GHAFUWRU
(Mwingi wa kusamehe), ASHAKUWRU (Mwenye kushukuru), AL-
`ALIYYU (Aliye juu), AL-KABIYRU (Aliye mkuu), AL-HAFIYDHU
(Mwenye kuhifadhi), AL-MUQIYTU (Mlinzi), AL-HASIYBU (Mwenye
kuhesabu), AL-JALIYLU (Wa hali ya juu), AL-KARIYMU (Mkarimu wa
hali ya juu), ARRAQIYBU (Mchungaji), AL-MUJIYBU (Mwenye kujibu),
AL-WAASI`U (Mwenye wasaa), AL-HAKIYMU (Mwenye hekima), ALWADUWDU
(Mwenye kupenda waja Wake), AL-MAJIYDU (Mwenye
utukufu), AL-BAA`ITHU (Mfufuaji), ASHAHIYDU (Mwenye kushuhudia
kila kitu), AL-HAQQU (Wa Haki), AL-WAKIYLU (Mtegemewa), ALQAWIYYU
(Mwenye nguvu), AL-MATIYNU (Aliye madhubuti), ALWALIYYU
(Mlinzi na Msaidizi), AL-HAMIYDU (Mwenye kusifika na
kila sifa njema), AL-MUHSIYU (Mwenye kuhesabu), AL-MUBDI-U
(Mwenye kuanzisha), AL-MU`IYDU (Mwenye kurejeza), AL-MUHYIYU
(Mwenye kuhuisha), AL-MUMIYTU (Mwenye kufisha), AL-HAYYU
(Mwenye uhai wa milele), AL-QAYYUWMU (Msimamia kila jambo), ALWAAJIDU
(Mtambuzi), AL-MAAJIDU (Wa kuheshimiwa), ALWAAHIDU
(Mmoja tu), ASSAMADU (Mwenye kukusudiwa kwa
kuabudiwa), AL-QAADIRU (Mwenye uwezo wa kufanya au
kutokufanya), AL-MUQTADIRU (Mwenye uwezo wa pekee juu ya kila
kitu), AL-MUQADDIMU (Mwenye kutanguliza), AL-MU-AKHIRU
(Mwenye kuakhirisha), AL-AWWALU (Wa Mwanzo), AL-AAKHIRU
(Wa Mwisho), ADHAAHIRU (Wa Dhahiri), AL-BAATINU (Wa Siri), ALWAALIYA
(Mpanga mipango ya watu), AL-MUTA`AALI (Mtukufu
Aliye juu), AL-BARRU (Mwema), ATTAWWAABU (Mwenye kupokea
toba za waja Wake), AL-MUNTAQIMU (Mlipa kisasi kwa waovu), AL-
`AFUWWU (Mwenye kusamehe madhambi), ARRAUFU (Mwenye
huruma), MAALIKU L-MULKI DHUL JALAALI WAL IKRAAMI
(Mfalme wa wafalme Mwenye utukufu na heshima), AL-MUQSITU
(Mtoaji haki sawa kwa kila anayestahiki), AL-JAAMI`U (Mkusanyaji
viumbe siku ya Mwisho), AL-GHANIYYU (Tajiri), AL-MUGHNIYU
(Mwenye kutajirisha), AL-MAANI`U (Mwenye kuzuia viumbe
visidhurike), ADHAARRU (Mwenye kudhurisha), ANNAAFI`U (Mwenye
kuleta nafuu), ANNUWRU (Mwenye nuru), AL-HAADIY (Mwongozaji
wa kheri), AL-BADIY`U (Mzuaji), AL-BAAQIYU (Mwenye kubakia
milele), AL-WAARITHU (Mwenye kurithi kila kitu), ARRASHIYDU
(Mwenye kuongoa waja kuiendea njia ya kheri), ASSABUWRU (Mwenye
kusubiri).”
Source /chanzo kutoka……
http://sekenke.com/bodi/showthread.php?t=190

About Me

Powered by Blogger.

Muda


Daily Hadith

Aya ya Quran

TAREHE


Kila siku Aya ya Qur'an